GAMONDI: SINA HARAKA KONKONI ATAKUA BORA TU

KOCHA MKuu wa Yanga raia wa Argentina Miguel Gamondi amesema kuwa hana haraka na straika wake Mghana Hafiz Konkoni kwani anaamini kuwa atampa anachotaka.

Gamondi alisema, anafahamu kuwa mchezaji huyo ni mzuri na ndiyo yupo kwenye klabu hiyo ila kwa sasa anahitaji muda kidogo ili kuweza kuwa bora na kufunga mabao kama ambavyo anatakiwa kufanya.KONKONIMiguel Gamondi alisema: “Sina shida na Konkoni, ni mchezaji mzuri ambaye kwa sasa anahitaji muda kuweza kutoa kitu ambacho watu wanahitaji. Najua mashabiki bado hawajapata kitu bora sana kutoka kwake.

“Ili aweze kufika huko anahitaji muda na ndiyo maana nimekuwa nikimpa nafasi yeye pamoja na wenzake wote kwenye kikosi.”GAMONDIKonkoni amecheza mechi mbili za ligi kuu na kufunga bao moja, lakini bado kumekuwa na mashaka kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakitarajia mabao mengi kutoka kwake.

Acha ujumbe