Chelsea Mawindoni kwa Kiungo Arsenal

Klabu ya soka ya Chelsea inataka kuongeza nguvu kwenye safu yake ya kiungo na mchezaji wanaemuwinda ni kiungo wa majirani zao klabu ya Arsenal Emile Smith Rowe raia wa kimataifa wa Uingereza.

Chelsea wanafanya mazungumzo na klabu ya Chelsea kwajili ya kuangalia uwezekano wa kumpata Emile Smith Rowe kwajili ya kuboresha safu yao ya kiungo ambayo wameshafanikiwa kusajili wachezaji kadhaa lakini Smith Rowe huduma yake inahitajika darajani.chelseaKiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua akikosa nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha Washika mitutu katika misimu miwili iliyomalizika na mpaka wakati huu hivo hii inaweza kumfanya kushawishika na kujiunga na matajiri hao wa jiji la London.

Klabu ya Arsenal inaweza kukubali kumuachia kiungo huyo kama The Blues watafikia dau ambalo wamelihitaji, Lakini pia kiungo Smith Rowe amekua hapati nafasi mara kwa mara kwenye timu hiyo hivo inaweza kuwafanya Arsenal kukubali kumuachia.chelseaKlabu ya Chelsea watahitaji kuhakikisha wanakamilisha usajili wa Smith Rowe ndani ya siku hizi zilizobakia kuelekea kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili majira haya ya kiangazi kama watafanikiwa kumsajili kiungo huyo atakwenda kuungana na Viungo kama Enzo Fernandez, Romeo Lavia, na Conor Gallagher.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.