Aston Villa Wanamtaka Lenglet

Klabu ya Aston Villa ipo kwenye mazungumzo na mabingwa wa soka nchini Hispania klabu ya Barcelona kwajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Clement Lenglet.

Aston Villa wanamuhitaji Clement Lenglet kwa mkopo wa msimu mzima huku wakiahidi kuhakikisha wanamlipa beki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa mshahara wake na Barcelona kutohusika kwenye suala hilo.aston villaBeki Clement Lenglet kama dili lake la kujiunga na Villa litakamilika atakua anatolewa kwa mkopo kwa msimu wa pili mfululizo kwani msimu uliomalizika alikua kwa mkopo klabu ya Tottenham Hotspurs.

Beki Clement hakua na msimu mbaya ndani ya klabu ya Tottenham msimu uliomalizika na ndio sababu kocha Unai Emery ameona kama mchezaji huyo anaweza kua moja mtu anaeweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.aston villaKlabu ya Aston Villa ni moja ya vilabu ambavyo vimefanya usajili mzuri katika dirisha hili la kiangazi na wanaendelea kuhakikisha wanaongeza watu kwenye kikosi chao kabla dirisha halifungwa ikiwa imebakia siku mbili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.