Aston Villa ya Unai Yamotoo

Klabu ya Aston Villa chini ya kocha Unai Emery imeonekana kua tishio kutokana na ubora ambao inauonesha katika kila mchezo na leo wamefanikiwa kupata matokeo ya ushindi wakiwa ugenini dhidi ya Burnley.

Aston Villa wameshinda mabao matatu kwa moja katika moja ya viwanja vigumu vya ugenini Turf Moore ambao ni uwanja wa nyumbani wa Burnley ambao wamekubali kichapo mabao matatu kwa moja kutoka kwa Villa.aston villaVijana wa Unai Emery wanashinda mchezo wa pili mfululizo kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo dhidi ya klabu ya Newcastle lakini baada ya mchezo huo hawajapoteza mchezo hata mmoja tena.

Ushindi wa Aston Villa ulipatikana kupitia magoli ya beki Matty Cash aliekua na mchezo mzuri kabisa akifanikiwa kufunga mabao mawili katika mchezo huo, Huku kiungo mpya wa klabu hiyo Moussa Diaby akifanikiwa kufunga bao la tatu.aston villaKlabu ya Burnley wao hawajafanikiwa kushinda mchezo wowote wa ligi kuu ya Uingereza na wakiwa wamefungwa michezo yote miwili ambayo wamecheza, Hii sio dalili nzuri kwa kikosi cha nahodha wa zamani wa klabu ya Man City Vicent Kompany.

Acha ujumbe