Manchester City Yajitoa kwa Nunes

nunes

Manchester City wako tayari kuachana na mpango wa kumsajili mchezaji Matheus Nunes kutoka Wolves. Meridianbet wakali wa odds kubwa kila jamvi ushindi ni uhakika.

Nunes amekataa kufanya mazoezi  lakini Wolves wanataka zaidi ya £60m na ​​inafahamika kuwa City hawataki kulipa zaidi ya £55m kama uhamisho wa mchezaji huyo.

Kiungo huyo wa kati wa Ureno hakuwa sehemu ya kikosi cha Gary O’Neil kilichopata ushindi wa kwanza msimu huu wikendi iliyopita, baada ya kufungiwa kwa kadi nyekundu aliyopokea katika kipigo cha klabu hiyo dhidi ya Brighton.

Pep Guardiola kwa muda mrefu amekuwa akimpenda Nunes, na ameanza maandalizi ya kuongeza kiungo baada ya nyota Kelvin De Bruyne kukosekana mapema mwezi huu.

Fukuzia ushindi unapoweka dau lako dogo la Tsh 250/= na kupata ushindi mkubwa.

Lucas Paqueta alikuwa ameibuka kwenye rada za mabingwa hao wa Premier League, lakini uhamisho wake kutoka West Ham uliporomoka baada ya kubainika kuwa alikuwa chini ya uchunguzi wa FA kuhusu uwezekano wa ukiukaji wa kamari.

Nunes alijiunga na Wolves kutoka Sporting Lisbon miezi kumi na miwili tu iliyopita, huku bosi wa wakati huo Bruno Lage akimsajili kwa ada ya rekodi ya kilabu ya £42m.

Acha ujumbe