Martial Alikuwa Anamchukia Mourinho?

Nyota wa Marchester United Anthoy Martial ameendelea kuwa mmoja ya wacjhezaji ambao wamekuwa na nguvu mpya na jitihada zaidi tangia Ole Gunnar alipompokea kwa mda aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho ambaye alitimuliwa kabla ya mwaka 2018 kuisha. Unafikiri nyota huyu alikuwa anamchukia Mourinho?

Sio rahisi kusema moja kwa moja, lakini bila shaka kuna baadhi ya wachezaji Manchester United walikuwa tayari wanapishana na aliyekuwa meneja wao Mourinho wakiwa hawafurahii kucheza chini yake. Paul Pogba ni mmoja wa wachezaji ambao bila shaka hawakufurahia kucheza chini ya meneja huyu aliyetimuliwa katika dakika zake za mwisho kulingana na kuzorota kwa uhusiano baina yao huku meneja huyo akimtaja kuwa Pogba hafai kabisa kuwa nahodha wa klabu hiyo.

Kwa upande wa Anthony Martial yeye alikuwa anasua sua kusaini mkataba mpya klabuni hapo. Nyota huyu wa miaka 23 mazungumzo juu ya mkataba wake yamedumu ndani ya miezi kadhaa tokea Mourinho alipokuwa klabuni hapo huku akihusishwa na kuihama klabu hiyo kama ambavyo wakala wake alijitokeza hadharani na kusema Martial alitarajia kuondoka klabuni hapo.

Kwa mujibu wa minong’ono ni kuwa hata nyota huyu kuna baadhi ya mazingira alikuwa anapoishana na Jose Mourinho, hata hivyo ripoti zinadai kuwa Mourinho alionekana kama mtu ambaye alikuwa anafurahia kuidhinisha kuondoka kwa nyota huyu pale United.

Kwa mujibu wa BBC, na taarifa ya hivi karibuni kutoka vyanzo vingine, Mashetani Wekundu wapo mbioni kukamilisha makubailiano ya dili mbya la mda mrefu la nyota huyu. Taarifa hizi zinaripoti kuwa Martial atakuwa amekamilisha maongezi ya Mkataba mpya Ijumaa. Sasa hapa unaweza kufikiria kuwa ile nia aliyokuwa ameishikilia mwanzo chini ya meneja Mourinho imefikia wapi, au lengo lake lilikuwa ni kuwa mbali na Mourinho lakini alikuwa na mapenzi na klabu hiyo.

Acha ujumbe