Mabingwa hawa wa ufaransa wanaonekana mambo si mambo katika League 1, Lakini Bosi wao mpya bwana Thomas Tuchel anajua kuwa Champions League ndio kipaumbele cha klabu hiyo.
Tangia klabu hiyo ilipofika mikononi kwa mamilionea wa Qatar mwaka 2011, wamefikia robo fainali mara 4 na pia 16 za mwisho mara 2, sasa wanataka wafikie nusu fainali na zaidi.
Baada ya kushinda mara tano katika mataji 6 yaliyopita ya League 1 na makombe yote ya nyumbani kwa misimu 4 iliyopita, wanahitaji kutoboa Zaidi.
Mifumo anayoipenda Tuchel
Bosi huyu mjerumani amejaribu mifumo ya 4-3-3, 3-4-1-2 na 4-2-3-1 tangu alipofika hapo Parc des Princes. Daily Star wameripoti kuwa licha ya ugumu wa kujua ni mfumo gani hasa atautumia kwa sasa, anaripotiwa kuwa 4-2-3-1 ndio silaha yake dhidi ya Liverpool.
Mfumo huu unaweza kuwa rafiki, baadhi ya wachezaji wanaikosa gemu dhidi ya Liverpool -Marco Verratti, Gianluigi Buffon, Dani Alves na Layvin Kurzawa wanatarajiwa kukosa gemu hiyo kwa sababu tofauti tofauti.
Mfumo unaotazamiwa kutumika na PSG ni (4-2-3-1): Areola; Meunier, T Silva, Kimpembe, Bernat; Marquinhos, Rabiot; Mbappe, Neymar, Di Maria; Cavani
Wataonekanaje Uwanjani?



Furahav
Mmh hatar.
Povel
Mfumo hatar sana huo
Fatina mfingi
Mmh