Arda Guler Haondoki Real Madrid

Klabu ya Real Madrid imeweka wazi kua haina mpango wa kumtoa kwa mkopo kinda wake raia wa kimataifa wa Uturuki mwenye kipaji kikubwa Arda Guler licha ya maombi ya vilabu mbalimbali.

Arda Guler amekua akihusishwa mara kwa mara kuondoka klabuni hapo kutokana na ufinyu wa nafasi ambao amekua akikutana nao, Lakini mabingwa hao wa ulaya wameweka wazi hawana mpango wa kumuachia.Arda GulerVilabu mbalimbali vimetuma maombi ya kumuhitaji kijana huo mwenye umri wa miaka (19) raia wa kimataifa wa Uturuki moja ya vilabu hivo ni klabu ya Getafe inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania.

Kwa upande wa mchezaji vilevile inaelezwa hana mpango wowote wa kutimka ndani ya Real Madrid licha ya tetesi zilizokua zinaenea kua anataka kutimka klabuni hapo ili akapate nafasi zaidi ya kucheza, Huku wakala wake akieleza hawajawahi kufikiria kuondoka ndani ya klabu hiyo.Arda GulerKiungo Arda Guler inaaminika anaamini kua anaamini ana  nafasi ya kuendelea kuipambania namba ndani ya klabu ya Real Madrid, Hivo hana mpango wa kutimka klabuni hapo akiamini kua wakati wake utafika na ataipambania klabu hiyo kwakua ndio malengo yake makubwa haswa kuelekea msimu wa 2024/25.

 

Acha ujumbe