Courtois Kufanyiwa Upasuaji

Golikipa wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois imefahamika amepata majeraha ya goti ambayo yatamfanya kufanyiwa upasuaji.

Golikipa Courtois amepata majeraha hayo wakati klabu hiyo ikiwa mazoezini leo kujiandaa na msimu mpya na kumfanya kipa huyo kuondka katika viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo na taarifa ya klabu kueleza golikipa huyo atafanyiwa upasuaji.CourtoisTaarifa zilitoka ni kua golikipa huyo atafanyiwa upasuaji ambapo taarifa ya kua golikipa huyo atakaa nje ya uwanja kwa muda gani bado haijafahamika, Lakini vyanzo mbalimbali vinaeleza anaweza kuukosa karibia msimu wote unaofuata.

Golikipa Courtois amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Real Madrid na kusimama kama moja ya walinda milango bora sana barani ulaya, Hivo golikipa namba mbili wa klabu hiyo Lunin raia wa Ukraine atakua golini kwa kipindi hichi.CourtoisTaarifa zingine ndani ya klabu ya Real Madrid zinasema klabu hiyo ina mpango wa kuingia sokoni kutafuta golikipa mpya, Kwani inawezekana golikipa huyo akakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi.

Acha ujumbe