Pedri: Nahitaji Kuwepo Barca

Kiungo wa klabu ya Fc Barcelona Pedri Gonzalez amesema anahitaji kuwepo ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu licha ya kuhusishwa kutakiwa na klabua ya PSG ya nchini Ufaransa.

Pedri wakati anazungumza na waandishi wa habari na kuulizwa kama anahitaji kutimka ndani ya klabu hiyo na kujiunga na klabu ya PSG, Kiungo huyo alieleza hana mpango wa kutimka ndani ya timu hiyo na mipango yake ni kusalia ndani ya timu hiyo.pedriKlabu ya PSG mwishoni mwa wiki iliyomalizika ilikua inahusishwa na kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania anayekipiga ndani ya klabu ya Barcelona, lakini kiungo huyo amekanusha taarifa hizo na kusema ni tetesi tu.

Kiungo huyo amekua  kwenye kiwango bora sana tangu apewe nafasi kwa mara ya kwanza kwenye timu ya wakubwa ya Barcelona akitokea akademi ya klabu hiyo na kugeuka kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya timu.Kiungo Pedri Gonzalez anasema mpango wake mkubwa ni kucheza ndani ya klabu ya Barcelona kwa miaka mingi zaidi na kuja kua nahodha wa klabu hiyo kubwa ulimwenguni, Lakini pia anahitaji kuja kucheza katika dimba jipya la klabu hiyio Spotify Nou Camp.

Acha ujumbe