Kiungo wa klabu ya Fiorentina ya Italia pamoja na timu ya taifa ya Morocco Sofyan Amrabat inaripotiwa anaitaka klabu ya Manchester United kuelekea msimu ujao.
Kuna taarifa zilikua zinaenea usiku wa jana kua kiungo Amrabat anataka kubaki ndani ya klabu ya Fiorentina, Lakini taarifa za kweli zinaeleza kiungo huyo anajiandaa kutimka klabuni hapo na uelekea wake ni klabu ya Man United.
Klabu ya Manchester United ilikua imetolea macho zaidi nafasi ya ushambuliaji wiki mbili zilizopita na sasa wameshafanikiwa baada ya kumnasa Rasmus Hojlund, Hivo kutokana na kumaliza suala hilo kwasasa watahamia kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco.
Taarifa kutoka katika kambi ya Amrabat zinaeleza kiungo huyo ameshakubaliana na klabu ya Manchester United maslahi binafsi, Hivo kinachochelewesha dili hilo ni klabu hiyo kutuma ofa rasmi kwa klabu ya Fiorentina.
Manchester United wanataka kuongeza wigo wa kikosi chenye ubora kwa kusajili wachezaji wenye ubora mkubwa kwenye kila eneo kiwanjani na ndio sababu wanamuhitaji kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco mwenye uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo wa ulinzi.

