Amrabat na United Mambo Mazuri

Kiungo wa klabu ya Fiorentina Sofyan Amrabat na klabu ya Manchester United wako kwenye hatua nzuri ya mazungumzo ili kukamilisha usajili wa kiungo huyo.

Manchester United wanaelezwa kumalizana na Amrabat kwenye maslahi binafsi, Huku klabu ya Fiorentina ikisubiri ofa kwa mchezaji huyo ili kuangalia kama itakua inakidhi vigezo vyao ili kumuachia mchezaji huyo.AmrabatKlabu ya Manchester United kipaumbele chao cha kwanza kwasasa ni kupata mshambuliaji ambaye ni Rasmus Hojlund kutoka klabu ya Atalanta, Lakini pia wanafanyia kazi suala la kiungo wa ulinzi mbadala wa Casemiro.

Sofyan Amrabat amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu ya Fiorentina na timu yake ya taifa ya Morocco, Hivo kuvivutia vilabu mbalimbali barani ulaya lakini Manchester United wakielezwa kuongoza mbio hizo.AmrabatKiungo huyo wa kimataifa wa Morocco inaelezwa sababu kubwa ya kukubali kujiunga na klabu ya Manchester United ni kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag, Kwani kocha huyo amewahi kumfundisha kiungo miaka mingi iliyopita katika klabu ya Utrech ya nchini Uholanzi.

Acha ujumbe