Barcelona Wamalizana na Balde

Klabu ya Fc Barcelona imefanikiwa kumalizana na beki wake kinda Alejandro Balde mwenye umri wa miaka 19 ambapo amesaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Beki Alejandro Balde amekubali kusaini kandarasi ya miaka mitano ya kuendelea kuitumikia klabu ya Barcelona mpaka 2028, Beki huyo kinda amekua mwenye uwezo mkubwa sana msimu uliomalizika ndani ya klabu hiyo.BarcelonaBaada ya kuondoka kwa beki Jordi Alba ndani ya viunga vya Camp Nou ni wazi beki Alejandro Balde ndio anaenda kuvaa viatu vya mkongwe huyo aliyefanya makubwa ndani ya klabu hiyo na hii ni kutokana na ubora wa kijana huyo ambao amekua anauonesha.

Klabu ya Barcelona ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha kua klabu hiyo inarejea kwenye ubora wake ambao imekua nao kwa miaka mingi, Hivo inalazimika kutengeneza timu mpya ya  vijana wenye uwezo kama kina Balde.BarcelonaAlejandro Balde sasa ataungana na vijana wenzake kama kina Pedri, Gavi Yamine Jamal, na Victor Roque ambao wapo kwenye mkakati mpya wa kuirudisha klabu hiyo juu kama ambavyo ilikua ikifanya vizuri miaka kadhaa iliyopita ambapo sasa wanaonekana kushuka ubora.

Acha ujumbe