Southampton Wataka Paundi Milioni kwa Lavia

Klabu ya Southampton ambayo imeshuka daraja kwasasa inataka kiasi cha paundi milioni 50 ili kumruhusu kiungo wake Romeo Lavia kutimka klabuni hapo.

Klabu ya Liverpool imefanya mazungumzo na klabu ya Southampton mapema leo kwajili ya kiungo Romeo Lavia ambapo klabu hiyo imedai inahitaji kiasi cha paundi milioni 50 ili iweze kumuachia kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji.southamptonLiverpool ni klabu ambayo imekua ikivutiwa na kiungo Romeo Lavia na yupo kwenye orodha ya juu kabisa ya viungo ambao klabu hiyo inawahitaji kuelekea msimu ujao hivo watahitajika kulipa kiasi cha pesa ambacho klabu ya Sotton wameulizia.

Kiungo Romeo Lavia amekua akifukuziwa na klabu ya Arsenal pia lakini mpaka sasa Liverpool ndio wameonekana mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaipata saini ya kijana huyo mwenye uwezo wa kipaji cha hali ya juu.southamptonSouthampton mpaka sasa wanaelezwa hawajapanga kushusha bei waliyoitaja kwa kiungo huyo, Huku wakijua kabisa klabu ya Liverpool wana shida ya kiungo kwani Jordan Henderson ameshatimka klabuni hapo na Fabinho naye yuko mbioni kuondoka.

Acha ujumbe