Villarreal Waachana na Setien

Klabu ya Villarreal imeamua kachana na kocha wake Queque Setien baada ya mfululizo wa matokeo mbaya ambayo yamekua yakiiandama klabub hiyo.

Villarreal imepoteza michezo yake mitatu kati ya minne ya ufunguzi ya ligi kuu ya Hispania msimu huu jambo ambalo limefanya uongozi wa klabu hiyo kufikiria kuachana na kocha huyo wa zamani wa klabu ya Fc Barcelona.villarrealKocha Setien aliichukua timu hiyo baada ya aliyekua kocha wa klabu hiyo Unai Emery kutimkia klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza katikati ya msimu uliomalizika na kuiongoza timu hiyo kupata matokeo mazuri.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo anayefahamika kwa jina la Miguel Angel Tena ataisimamia kwa muda klabu hiyo, Huku klabu hiyo ikiwa inafanya utaratibu wa kutafuta kocha mwingine kwajili ya kuiongoza klabu hiyo.villarrealVillarreal imeanza msimu ikiwa haina matokeo ya kuridhisha na ndio sababu ya kumuondoa kocha Setien, Klabu hiyo imefanikiwa kusajili wachezaji kadhaa wenye uwezo hivo matokeo mabaya klabuni hajayawavutia viongozi wa timu hiyo.

Acha ujumbe