Amrabat Atambulishwa Rasmi Man United

Kiungo mpya wa klabu ya Manchester United Sofyan Amrabat ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea klabu Fiorentina kwa mkopo wa mwaka mmoja ambapo ametambulishwa rasmi klabuni hapo leo.

Amrabat ambaye alisajiliwa kwa siku ya mwisho ya usajili ameweza kutambulishwa leo katika viunga vya Old Trafford, Huku kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco akikabidhiwa jezi namba nne iliyokua ikivaliwa na beki Phil Jones.amrabatKiungo huyo ambaye alikua anasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa klabu hiyo, Kwani wanaamini anaweza kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo msimu tena kutokana na mwanzo wa kusuasua walioanza nao klabu hiyo.

Kiungo Amrabat ni usajili unaoonekana wa tija sana ndani ya klabu ya Manchester United, Kwani kiungo ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti tofauti kwenye eneo la katikati na kuzingatia kipindi hichi ambacho Casemiro hana kasi kama aliyokua nayo msimu uliomalizika.amrabatKlabu ya Manchester United wamemsajili kiungo huyo kutoka Fiorentina ya nchini Italia kwa mkopo wa msimu mzima, Lakini kuna kipengele cha kuweza kumnunua kwa uhamisho wa kudumu baada ya mkataba huo kumalizika.

 

Acha ujumbe