Bukayo Saka alicheka baada ya kulinganishwa na supastaa wa Ufaransa Kylian Mbappe, akisisitiza kuwa ‘kuna Mbappe mmoja tu, na saka mmoja tu’ kabla ya timu zao kukutana katika robo fainali ya Kombe la Dunia Jumamosi.

Uingereza ilijikatia tiketi ya kucheza mechi ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Al Bayt kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Senegal, huku Saka akifunga bao la mwisho la England usiku huo.
Bukayo saka anashikilia nafasi ya 5 kwenye orodha ya wafungaji wa kombe la dunia akiwa na mabao 3, nafasi tatu nyuma ya mfungaji bora Mbappe mwenye jumla ya mabao 5, lakini mazungumzo yoyote ya kufananishwa na supastaa huyo wa Paris Saint-Germain yamepingwa vikali na Bukayo Saka mwenyewe.
Alipoulizwa kama yeye ni Mbappe wa Uingereza, alisema: “Asante, lakini hapana. Nadhani kuna Mbappe mmoja tu na mimi ni mmoja tu.

“Nataka tu kuisaidia timu yangu. Kuna wachezaji wengi vijana wanaofanya vizuri, wakiwemo katika timu yetu. Kipaumbele ni kushinda mashindano, si mchezaji bora wa mashindano, au mchezaji mdogo wa mashindano.”
Hii ni mara ya kwanza kwa Saka katika Kombe la Dunia, lakini anaonekana kuwa bora zaidi kwenye mechi zote alizocheza.
Ufaransa, ambayo iliishinda Poland 3-1 katika hatua ya 16 bora ili kukata miadi na Uingereza, itawakilisha hatua kubwa ya ubora kwa Three Lions, lakini ushindani mkubwa kati ya mataifa hayo mawili unasisimua, badala ya kutisha.

