Wachezaji wa Brazil Rodrygo na Marquinhos wamewaonya wachezaji wenzao juu ya kujiamini zaidi kulekea Kombe la Dunia, huku wakiwa ni timu inayopigiwa chapuo na watu wengi kuwa na nafasi kubwa ya kuchukua Kombe hilo.

 

Rodrygo na Marquinhos Wawaonya Wenzao Dhidi ya Kujiamini Sana

Brazil wanajivunia kuwa moja ya timu kali kwenye karatasi, ikijumuisha wachezaji wa kiwango cha juu Duniani kama vile Neymar na Vinicius Junior, na wamefanikiwa kutinga fainali mbili za Copa America tangu Kombe la Dunia la 2018, wakishinda 2019 na kufungwa 1-0 na Argentina mnamo 2021.

Pia watacheza Kundi G, ambapo wataungana na Cameroon, Serbia na Uswizi katika mechi tatu ambazo Brazil inapendelewa zaidi kupita katika kundi hilo na kutinga katika hatua zingine zinazofuata.

Akizungumza na vyombo vya habari hapo jana Rodrygo ambaye anaichezea Real Madrid alisema ingawa anaelewa shinikizo la timu yake kucheza nchini Qatar, angependelea kuruhusu mchezo ndo uongee kama wanastahili chapuo hilo au laa.

Rodrygo na Marquinhos Wawaonya Wenzao Dhidi ya Kujiamini Sana

“Tunafahamu kuwa tuna timu kubwa ya Taifa, kwamba sisi ni miongoni mwa timu zinazopendwa, lakini pia kuna timu nyingine nzuri sana pia na haifai kusema sisi ni wapenzi wa watu halafu tufike uwanjani na tusionyoshe hilo.”

Rodrygo aliendelea kusema kuwa wanajua kwamba kila mmoja alikuwa katika hali nzuri na vilabu vyao na ndiyo maana waka hapo, pia kuna wachezaji wengi wazuri wameachwa. Naye beki wa kati wa PSG Marquinhos amekubali, akisema watahitaji kucheza kwa uchu ili kutimiza malengo yao.

Marquinhos alisema kuwa ikiwa wao ni vipenzi vya watu kuelekea Kombe hilo, basi watahitaji kuongeza jitohada kwani emeona mambo yalivyo katika mashindano haya ambayo ni magumu sana, na timu zote zipo tayari na zina uwiano mzuri, zinaweza kufanya maisha kuwa magumu. Hilo ndilo Kombe la Dunia.

Rodrygo na Marquinhos Wawaonya Wenzao Dhidi ya Kujiamini Sana

Haifai kuzungumza juu ya siku zijazo kwani lazima wapitie hatua ya makundi kwanza na itakuwa michezo mitatu migumu sana. Brazil wataanza Kampeni yao Alhamisi, Novemba 24 dhidi ya Serbia.

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Rodrygo, Rodrygo na Marquinhos Wawaonya Wenzao Dhidi ya Kujiamini Sana, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa