Mchezaji wa Real Madrid Rodrygo anaona kuwa kuchukua nafasi ya Kareem Benzema “haiwezekani” hata hivyo Mbrazili huyo anajitoa kwa hali na mali katika timu hiyo ili aweze kuziba pengo la Benzema ambaye ni majeruhi.

 

Rodrygo: "Haiwezekani Kuchukua Nafasi ya Benzema"

Bao la kwanza la Real Madrid lilifungwa na Rodyrgo katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Atletico Madrid Jumapili, huku vijana wa Carlo Ancelotti wakiendeleza rekodi yao ya asilimia 100 kwenye Laliga na kuwa kileleni kuelekea mapumziko ya Kimataifa.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Brazil  alishirikiana vyema na Aurelien Tchouameni nakupachika wavuni bao dakika ya 18, kabla ya Federico Valverde kufanya ubao kusomeka 2-0 kabla ya mapumziko.

 

Rodrygo: "Haiwezekani Kuchukua Nafasi ya Benzema"

Atletico walipambana na kupata bao katika dakika za lala salama kuptia kwa Mario Hermoso, lakini halikutosha kuamsha urejesho kamili. Wakati nahodha wa Real Madrid Benzema akitarajiwa kurejea uwanjani baada ya mapumziko ya Kimataifa, Ancelotti ameweza kumtegemea Rodrygo kuongoza safu ya ushambuliaji wakati Mfaransa huyo hayupo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amechangia mabao matano katika mechi nane za mwisho za Laliga  na alivyoulizwa katika mahojiano  baada ya mechi na Movistar+ ilikuwa ni vigumu kivipi kucheza bila Benzema alisema “Siku zote nimekuwa na imani lakini msimu uliopita nilifunga mabao mengi mwishoni mwa kampeni na sasa nimewafunga mwanzoni pia.

“Haiwezekani kuchukua nafasi ya Benzema, Lakininajaribu na ninadhani naendelea vizuri. Lazima niseme kwamba ninafanya mambo tofauti kwake, tumebadilisha mtindo wa uchezaj”.

 

Rodrygo: "Haiwezekani Kuchukua Nafasi ya Benzema"

Rodrygo na Madrid wameshinda mechi zao zote tisa msimu huu katika mashindano yote, na ndio timu pekee katika ligi tano bora za Ulaya yenye rekodi nzuri , ambapo inakuwa mara tatu kwa Madrid kushinda mechi tisa za kwanza katika kampeni moja baada ya 1961-62, na 1968-69 waliposhinda mechi 11 za ufunguzi katika kampeni zote mbili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa