Rodrygo Agoma Kufananishwa na Neymar.


Kinda wa Brazil, Rodrygo amesema hataki kuwa “Neymar mpya” wakati akifafanua kulinganishwa kwake na nyota huyo wa Selecao.

Rodrygo ni mmoja wa wachezaji wachanga wenye vipaji katika mpira wa miguu akiwa na mabingwa wa La Liga, Real Madrid, akipata kutambuliwa kama mshindi wa Tuzo ya Goal NxGn 2020.

 

 Rodrygo Agoma Kufananishwa na Neymar.

Winga huyo wa miaka 19 alihamia kwa Euro milioni 45 kutoka Santos kwenda Madrid mnamo 2019 na amekuwa akilinganishwa na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar na nyota wa Zamani wa Man City, Robinho, ambao wote walitokea katika klabu hiyo ya Brazil.

Amelinganishwa na Neymar tangu umri wa miaka 12, wakati aliposaini makubaliano na Nike kuwa mwanamichezo mdogo zaidi aliyewahi kudhaminiwa na kampuni hiyo.

Lakini Rodrygo hafurahii kulinganisha kwani yeye badala yake anatarajia kuunda njia yake mwenyewe, tofauti na hao wachezaji wengine.

 

 Rodrygo Agoma Kufananishwa na Neymar.

“Tangu mwanzo wa taaluma yangu wakati naanza Santos, tayari walinilinganisha kama “Neymar mpya” na Robinho. Siku zote nilisema kwamba ninataka kuwa Rodrygo na kutengeneza historia yangu”.

“Robinho na Neymar ni wa kuigwa kiasi kikubwa kwa Santos na kwa maeneo yote ambayo walicheza, nadhani kuna Neymar mmoja tu”. alisema mchezaji huyo.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

23 Komentara

    Safi sana Rodrygo.tafuta njia yako.na sio kufananishwa na mtu

    Jibu

    kila mtu ana kiwango chake na uwezo wake awapo uwanjani kufananishana si jambo zuri

    Jibu

    kiwango alichokua nacho Rodrygo cha kawaida tu hawezi kumfikia neyrma

    Jibu

    Hapana bado ajamfikia neyrma

    Jibu

    Anataka kuwa wa kipekee zaidi

    Jibu

    Hataki kufananishwa kwa sababu hawezi kuwa kama neyrma

    Jibu

    Bado hawezi kumfikia Neymar

    Jibu

    Nakala nzuri #meridianbettz

    Jibu

    Vizuri kilamtu anaupeo wake wakifikra kwaiyo yeye ataki kufananishwa na mtu

    Jibu

    Rodrygo amekuwa muwazi kuwa Neymar ni mchezaji wa kuigwa ila hataki kufananishwa nae,anataka kujijengea ufalme wake

    Jibu

    yupo sahihi anataka kua yeye kama yeye na sio kufananishwa

    Jibu

    Kwa kuwa sio kipofu lazim atembee anavyojua pongz sna Rodrygo

    Jibu

    Rodrygo yupo sahihi ataki kufananishwa na kitu chochote

    Jibu

    Neymar ni mchezaj makin sana

    Jibu

    Rodrygo hawezi kufikia kiwango hicho cha Neymar

    Jibu

    hawezi kumfikia Neymar

    Jibu

    Ni mapema kumfanishana neymar sema tumpe muda spoon hanawez kufik level ya neymar

    Jibu

    Anajua Bado hajafikia kiwango cha Neymar

    Jibu

    Hapo ni vitu viwili tofauti

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Wivu tu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.