Kocha wa AS Roma Jose Mourinho amepewa kadi nyekundu baada ya kupata hasira zaidi baada ya timu yake kukataliwa penati katika dakika ya 55 huku timu yake ikipoteza mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Atalanta kwenye Serie A.

 

Mourinho Apewa Kadi Nyekundu

 

Kocha huyo alikuwa na hasira zilizopitiliza kutokana na kitendo hicho wakati Nicolo Zaniolo alipotoka nje chini ya changamoto ya Caleb Okolo  na wakati video ya marudiano ilipoonyeshwa ilionekana kuwa wachezaji wote wawili walikuwa wakigombania jezi ya kila mmoja wao kwa muda mrefu kabla ya Zaniolo kwenda chini, na mwamuzi Daniele Chiffi akapuuza rufaa hiyo.

Na ndipo Mourinho akaungana na wachezaji wake kupinga uamuzi huo, akikimbia uwanjani na kupiga kelele na kumnyooshea kidole Chiffi, kabla ya mwamuzi kuonyesha kadi nyekundu. Bao pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na Scalvin wa Atalanta dakika ya 35 na ndilo lilidumu hadi kumalizika kwa mchezo huo.

 

Mourinho Apewa Kadi Nyekundu

Roma sasa wamepoteza mechi mbili kati ya tatu zilizopita za Serie A, idadai kubwa ya vipigo kama walivyopata katika mechi 21 zilizopita ambapo walishinda mechi 11 wakatoa sare 8  ambapo wanashika nafasi ya 6 katika msimamo baada ya mechi saba za raundi hii.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa