Klabu ya Brighton imemtambulisha kocha mpya anayejulikana kwa jina la De Zerbi kuinoa timu hiyo baada ya aliyekuwa kocha wao Graham Potter kujiunga na Chelsea wiki chache zilizopita.

 

Brighton Yamtambulisha Kocha Mpya

 

Muitaliano huyo ametajwa kuwa mrithi wa Graham Potter baada ya kuweka wino kwenye karatasi kwenye mkataba wa miaka minne katika uwanja wa Amex Stadium siku ya Jumapili. De Zerbi anachukua mikoba ya Potter kufuatia kwa mwendelezo mzuri wa kikosi hicho huku kutwaa alama 13 katika mechi 6 walizocheza.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43, alikuwa hana kazi tangu aondoke Shakhtar Donetsk mwezi Julai kwasababu ya vita vua Ukraine, ataanza kuinoa Brighton ugenini ambapo watakuwa wakicheza dhidi ya Liverpool mwezi Oktoba.

Mwenyekiti wa Brighton Tonny Bloom aliiambia tovuti rasmi ya klabu  “Nimefurahi sana Roberto amekubali kuwa kocha wetu mpya, Timu za Roberto zinacheza soka la kusisimua na la kijasiri, na nina imani mtindo wake na mbinu yake itakidhi kikosi chetu kilichopo kwa kiasi kikubwa”

 

Brighton Yamtambulisha Kocha Mpya

De Zerbi analeta pia uzoefu wa Serie A kwenye Dimba la Brighton akiwa amesimamia Palermo, Benevento, na Sassuolo katika ligi kuu ya Italia.  Kiungo huyo wa zamani wa Milani na Napoli aliiongoza Sassuolo kumaliza katika nafasi ya nane mfululizo katika kipindi chake cha miaka mitatu akiwa na timu hiyo ya Italia.

Brighton mpaka sasa inashikilia nafasi ya nafasi ya 4 akiwa na point 14 huku akiwa ameshinda mechi nne, amesare moja na amepoteza moja na mechi ijayo atamfata Liverpool Anfield.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa