Klabu ya Juventus wameendelea kua na mfululizo wa matokeo mabaya baada ya kupoteza mchezo tena leo dhidi ya timu iliopanda daraja msimu huu huko nchini Italia.

Miamba hiyo iliyopo chini ya mwalimu Massimiliano Allegri imeonekana kuchechemea zaidi msimu huu kwani mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo miwili na kusuluhu michezo minne huku wakipoteza mchezo mmoja katika ligi hiyo kwenye michezo saba waliocheza mpaka sasa huku wakiwa wamekusanya alama 10 na kudoshosha jumla ya alama 11 wakikamata nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu nchini humo.

juventusKikosi hicho kimekua na wakati mgumu kipindi ambacho kimefanikiwa kuongeza wachezaji kadhaa kwenye kikosi na wenye ubora kama Paul pogba,Angel di maria,Leandro parades pamoja na beki raia wa Brazil Bremer kutoka klabu ya Torino ila inaonekana kutokubadilisha chochote kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Turin.

Kwenye mchezo wa leo ambao Juventus wamepigwa goli moja kwa bila walicheza pungufu muda mwingi wa mchezo baada ya mchezaji Angel di maria kupewa kadi nyekundu dakika 40 ya mchezo kipindi cha kwanza.

Wakati huohuo mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo amedai hawezi kumfukuza aliyeko kwasasa kwasababu wana mipango ya muda mrefu ambayo mwalimu huyo ndani ya hiyo mipango.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa