England: Mchezaji wa Arsenal Ethan Nwaneri amekuwa ndiye mchezaji mdogo zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Ligi kuu ya Uingereza kuwahi kucheza huku akiwa na miaka 15 ambapo hii leo amecheza kwenye mechi waliyokuwa wakikabiliana na Brentford ugenini.

 

Nwaneri Awa Mchezaji Mdogo Kabisa EPL.

Mchezaji huyo ametambulishwa hii leo ambapo aliingia katika kipindi cha pili cha mchezo huo ambao umemalizika kwa Arsenal kushinda mabao 3-0 huku wakipanda kileleni na kuongoza ligi kwa mara nyingine tena kwa alama 18.

Kikosi cha Mikel Arteta kilikuwa bila Martin Odegaard na Oleksandr Zinchenko kwa safari ya Brentford  Community Stadium, huku vijana Nwaneri na Lino Sousa wakitajwa kwenye benchi kwenye timu hiyo.

 

Nwaneri Awa Mchezaji Mdogo Kabisa EPL.

Zikiwa zimeongezwa dakika nne, Atrteta alimtumia Nwaneri kuchukua nafasi ya Vieira huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 akiweka jina lake katika historia ya ligi kuu. Kiungo huyo mwenye miaka 15 na siku 181, amekuwa mchezaji mdogo zaidi kushiriki  mechi za ligi kuu ya Uingereza na kuvunja rekodi ya Harvey Elliott ya miaka 16 na siku 30 kwa Fulham.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa