Tchouameni Amepuuzia Uvumi Unaoihusu Ufaransa na Benzema

Aurelien Tchouameni amepuuzi mbali mapendekezo ya kikosi cha Ufaransa kuwa mahali pazuri zaidi bila Karim Benzema baada ya kufika raundi ya mtoano ya Kombe la Dunia.

 

Tchouameni Amepuuzia Uvumi Unaoihusu Ufaransa na Benzema

Kikosi cha Didier Deschamps kimetinga hatua ya 16 bora huko Qatar 2022 baada ya ushindi dhidi ya Denmark katika Kundi D, huku Kylian Mbappe akifunga mabao mawili na kuifanya  Les Bleus kushinda 2-1 hapo jana.

Mshambuliaji huyo ameitumikia timu yake hadi sasa bila ya Benzema, huku mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or akitolewa katika usiku wa kuamkia michuano hiyo kutokana na jeraha la paja.

Baadhi ya ripoti zimesema kumekuwa na hali nzuri zaidi kutokana na kukosekana kwa nyota huyo wa Real Madrid, ambaye hakuhusika Urusi 2018, lakini Tchouameni sasa amejaribu kufuta uvumi huo.

Tchouameni Amepuuzia Uvumi Unaoihusu Ufaransa na Benzema

Tchouameni amesema kuwa; “Ninataka kurejea jambo tuliloona kuhusu kuondoka kwa Karim, mahali fualani tumejisikia bora kwa vile hayupo tena. Ni uongo kabisa, hata alipokuwa huko, tayari ilikuwa Ufaransa inaendelea vyema na tumeumizwa na ripoti hizi.”

Amesisitiza kusema kuwa tangu wamefika Qatar mambo yamekuwa yakienda vizuri tu huku akiwa ameshacheza mechi mbili mpaka sasa, Tchouameni anakuwa kiungo muhimu wa Deschamps katika kutetea ubingwa wa timu yake, huku Ufaransa pia ikiongezewa nguvu na kurejea kwa beki Raphael Varane.

Beki huyo wa kati wa Manchester United amekuwa akiuguza jeraha tangu mwishoni mwa Oktoba, lakini alirejea uwanjani kwa kuanza dhidi ya Denmark, akitafakari juu ya jeraha lake Varane amesema kuwa ametoka mbali, na imekuwa kazi kubwa jitihada nyingi kurejea.

Tchouameni Amepuuzia Uvumi Unaoihusu Ufaransa na Benzema

Varane amesema pia anajisikia vizuri, daima ni maalum kucheza kwenye tukio hili la kipekee na atatumia kila wakati kufanya kila kitu ili aweze kufika mbali iwezavyo, huku timu yake itarajia kumaliza kampeni ya Kundi D dhidi ya Tunisia mnamo Novemba 30, huku wakiwa tayari wameshatinga hatua ya 16 bora.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

KOMBE LA DUNIA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.