Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Aurelien Tchouameni amefunguka kua hakua na chaguo la lingine zaidi ya mabingwa hao wa ulaya pale walipohitaji huduma yake.

aurelien Tchouameni“Sikusita kwenda PSG ni klabu kubwa pia barani ulaya, lakini nilikua na chaguo moja tu nalo klabu ya Real Madrid” Alisema Aurelien Tchouameni.

Pia kiungo huyo alizungumzia suala la yeye kusajiliwa kwa dau kubwa ambalo wanadai sio thamani halisi kutokana na uwezo wake aliouonesha katika klabu ya As Monaco ya nchini Ufaransa “€80milioni? sikua ofisini kufanya majadiliano ya hiyo pesa kitu nachojua mimi ni kuja Madrid na kufanya kazi inatosha”.

Aurelien Tchouameni tangu atue katika klabu hiyo amekua akionesha kiwango cha hali ya juu na wengi wakiamini klabu hiyo imepata mbadala sahihi wa kiungo Carlos Casemiro alietimkia klabu ya Manchester united baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na Tchouameni anaonekana kama mbadala sahihi klabuni hapo.

 

aurelien tchouameniMchezaji huyo wa zamani wa klabu ya As Monaco aliekua akiwindwa na vilabu mbalimbali barani ulaya ila aliishia kutua kwenye viunga vya Bernabeu yalipo maskani ya klabu ya Real Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa