Aurelien Tchouameni ameanza vizuri ndani ya klabu yake mpya ya Real Madrid baada ya kuonesha kiwango bora.
Kiungo huyo raia wa Ufaransa ambaye amesajliwa dirisha hili la majira ya joto na mabingwa hao ulaya akitokea klabu ya As Monaco ameanza kuonesha uwezo aliokua nao ni wa hali juu na kuwafunga mdomo ambao walionekana kupinga kiasi kikubwa cha pesa alichonunuliwa nacho ndani ya klabu hiyo.
Aurelien Tchouameni kwenye michezo yote aliyoanza ndani ya Real Madrid msimu ameonesha kiwango kizuri ila gumzo ni michezo miwili ya mwisho dhidi ya Espanyol ugenini alikua na kiwango bora sana na aliweza kupiga pasi ya bao na mchezo wa leo dhidi Real Betis katiba dimba la Santiago Bernabeu ambapo Madrid wamefanikiwa kupata ushindi huku kiungo akiibuka kama nyota wa mchezo.
Kocha wa timu hiyo Carlo Anchelotti amesifia kiwango cha mchezaji huyo huku wengi wakiamini atakua kiungo bora sana siku za mbeleni.
Kiungo huyo amepata namba ya kudumu baada ya kuondoka kwa kiungo aliekua akicheza nafasi yake raia wa Brazil Carlos Casemiro akietimkia klabu ya Manchester United na kumpa nafasi kijana huyo kuonesha ubora wake.

