Madrid Yakamilisha Usajili wa Aurelién Tchouaméni.

 

Klabu ya Real Madrid imekamilisha rasmi usajili wa kiungo wa Monaco, Aurelién Tchouaméni kwa mkataba wa kudumu wa miaka sita pale Santiago Bernabeu.

Taarifa rasmi inathibitisha makubaliano kamili kati ya Real Madrid na AS Monaco kwa ada ya €80m pamoja na nyongeza karibu €20m.

 

Tchouaméni ametia saini kandarasi hadi Juni 2028 baada ya makubaliano binafsi kufikiwa wiki zilizopita, licha ya nia ya vilabu vingine kuhitaji huduma zake.

Vilabu vya Liverpool, Chelsea na Paris Saint-Germain walimtaka Aurelién lakini hajawahi kubadili mawazo yake juu ya kujiunga na Real pekee.

Tchouaméni atafanyiwa vipimo vya mwisho vya afya siku ya Jumanne kisha atawasilishwa rasmi Santiago Bernabéu kama mchezaji mpya wa Madrid.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.