Gian Piero Gasperini alisikitishwa zaidi kuliko kujivunia timu yake ya Atalanta kwa kushindwa kwao UEFA Super Cup dhidi ya Real Madrid. Akisema kuwa walikosa nafasi kubwa na wanapaswa kuwa wazuri zaidi.
Lilikuwa swali kubwa kila mara kwa La Dea kwenda kucheza na Galacticos kwenye Uwanja wa Taifa wa Warsaw, haswa baada ya kulazimishwa kucheza bila Gianluca Scamacca, Nicolò Zaniolo, Teun Koopmeiners, Giorgio Scalvini na Rafael Toloi.
Walipata nafasi hata hivyo, na bila ya Thibaut Courtois kuokoa mpira wa kichwa uliopanguliwa na Mario Pasalic, lakini muda mfupi baadaye Federico Valverde akafunga bao la kwanza, na kufuatiwa dakika tisa baada ya bao la kwanza la Kylian Mbappé.
“Nilikuwa na imani kwamba tunaweza kusababisha matatizo kwa Real Madrid na mtindo wetu wa soka. Ni wazi, mchezo ulibadilika baada ya bao lao, haswa lile la pili. Bila shaka walistahili ushindi huo,” Gasperini aliambia Sky Sport Italia.
Gasperini aliongeza kuwa walikuwa wameanza vyema kipindi cha pili na walipata nafasi hizo kubwa kutoka kwa Pasalic, lakini pia Lookman alikuwa ana mchezo mzuri hapo jana.
“Ni wazi, katika michezo hii yeyote anayeongoza anapata kasi na inakuwa vigumu kurejea, kama vile tulipotangulia mbele ya Dublin,” alisema Gasperini, akizungumzia ushindi wa Fainali ya Europa 3-0 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Hadi Gasperini alipofika, dhamira kubwa ya klabu hii ilikuwa kujaribu kusalia Serie A na hapa walikuwa kama mabingwa wa Ligi ya Europa, wakiwa wamecheza vyema kwenye UEFA Super Cup, lakini majibu yake yanaonyesha jinsi walivyofikia malemgo yao.
“Tulikosa nafasi kubwa ukizingatia jinsi mchezo ulivyokuwa unaenda na hilo linanikatisha tamaa. Tunapaswa kuwa wabunifu zaidi na kuonyesha ubora zaidi katika hali hiyo, kwani ilikuwa muhimu sana kushinda jana.”
Katika filimbi ya mwisho, wachezaji wa Atalanta walikwenda chini ya sehemu iliyokuwa na mashabiki takriban 6,000 waliofunga safari kutoka Bergamo na wakajiunga katika kushuhudia mchezo huo.
Ancelotti pia alizungumza na Gasperini kwa muda kabla ya kuvalishwa medali zao.
Nina maelewano makubwa na Carlo, tulizungumza kuhusu soka. Tunataka kuchukua kitu chanya kutoka kwa mchezo huu, kisha msimu wetu wa Serie A utaanza Jumatatu, ni mashindano tofauti sana na tutaona kitakachotokea. Alisema Gasperini.
“Kwa bahati mbaya, itabidi pia tuhesabu nani amesalia, kwa sababu Sead Kolasinac alitoka nje akiwa na jeraha.”