Klabu ya Geita Gold leo hii, imepata alama 3 kwa mara ya kwanza msimu huu toka wapande ligi kuu ya NBC, baada ya kucheza mechi 6 kitu ambacho msimu uliopita hakikuwepo.
Geita wamepata ushindi huo wakiwa ugenini,walipokuwa wakicheza dhidi ya Poilisi Tanzania ambapo walitangulia kupata goli la kwanza kupitia kwa George Mpole na baadae goli hilo kuja kusawazishwa katika dakika za 64.
Dakika ya 80 Geita Gold walipata adhabu ya kadi nyekundu, lakini dakika 3 baadae John akaifungia timu hiyo bao la kuongoza ambalo limeipa alama tatu na kuifanya timu hiyo ipande hadi nafasi ya 11 kwenye msimamo.
Mshambuliaji wa timu hiyo ambae ni George Mpole msimu uliopita ndiye alikuwa mfungaji bora akimpita Fiston Mayele, lakini mpaka sasa ndani ya mechi sita amefunga mabao mawili.