Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hakuna mchezaji anaeweza kushindana na mshambuliaji wake hatari Earling Haaland kwenye umri aliokua nao.

Kocha huyo amesema mshambuliaji huyo ameweka viwango ambavyo haviwezi kufikiwa na mchezaji mwingine mwenye umri wake kwasasa na kumtaka kuenelea kuimarisha kiwango chake ili kuendelea kua bora zaidi ya hapo alipo.

pep guardiolaMchezaji huyo ambaye alifunga magoli matatu na kupiga pasi mbili za mabao katika ushindi wa magoli sita kwa moja dhidi ya mahasimu zao klabu ya Manchester United siku ya jumapili na kumfanya mchezaji huyo kufikisha magoli 17 katika michezo 11 aliyoitumikia City tangu ajiunge nayo akitokea klabu ya Borussia Dortmund.

Akiwa na miaka 22 na siku 47 amefanikiwa kumpiku Klian Mbappe kwa kufikisha magoli 25 haraka zaidi akiwa na umri mdogo huku akiwa pia akiwa amecheza mechi chache zaidi (20).

Pep Guardiola anaamini namba zinajieleza zenyewe unapomuongelea Haaland na anatarajia kuongeza idadi ya mabao kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Fc Copenhagen.

“Katika umri wake hakuna anaeweza kushindana nae. Hakuna”, “Tuna furaha kubwa kua naye. katika mazoezi wakati mwingine anafanya mambo ya ajabu tuna furaha sana kua naye”Alisema Pep Guardiola

pep guardiola“Ni mchezaji wa pekee ambae amekua kwa haraka sana” Pep amezungumza hayo kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Fc Copenhagen.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa