Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema timu yake inapaswa kujiimarisha zaidi ya kuifunga klabu ya Manchester United mabao sita kwa matatu katika mchezo wa ligi ya kuu ya Uingereza uliopigwa katila dimba la Etihad.
Pep Guardiola na vijana wake walifanikiwa kuifunga United kipigo cha fedheha cha mabao sita kwa matatu huku Earling haaland pamoja Phil Foden wakifanikiwa kufunga magoli matatu kila mmoja katia mchezo huo.
Licha ya ushindi huo kocha huyo amesisitiza timu yake inahitaji kujiboresha zaidi kuelekea michezo ijayo ya klabu hiyo baada ya kupaya matokeo mazuri leo dhidi ya mahasimu wake katika jiji la Manchester.
Pep Guardiola pia hakuacha kusifu ubora wa wachezaji wake haswa kipindi cha kwanza cha mchezo walipoonesha ukatili zaidi wanapokua na mpira na kutengeneza nafasi za mabao na kuweza kuondoka na uongozi wa goli nne kwa bila.
Kocha huyo pia alisifu kiwango cha United katika kipindi cha pili cha mchezo baada ya klabu hiyo kupata mabao matatu huku City wakipata mabao mawili na kusema walicheza vizuri zaidi kipindi cha pili kuliko wao.