Klabu ya Juventus ya Italia imempunguzia presha kocha wao Massimiliano Allegri baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya Bologna wakiwa nyumbani kwao, huku mabao hayo yakitupiwa kimyani Filip Kostic, Dusan Vlahovic na Arkadiusz Milik.
Kuelekea mechi hiyo ya kikosi cha Massimiliano Allegri kilikuwa hakijashinda katika mashindano yote tangu mwisho wa Agosti, na kufanya kibarua cha kocha huyo kuwa hatarini.
Juventus imekuwa ikipitia wakati mgumu msimu huu, baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha, ambapo mpaka sasa yupo nafasi ya saba baada ya mechi nane alizocheza, huku nafasi ya kuwania nafasi ya ubingwa inazidi kuwa ngumu kwake.
Siku ya Jumatano Allegri atamkaribisha Maccabi Haifa kwenye mchezo wa Klabu Bingwa, baada ya kupoteza michezo yake yote miwili ya kwanza kwenye michuano hiyo.