Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema hawezi kumkosoa mshambuliaji wake  Karim Benzema baada ya kukosa penalti hapo jana ambayo penati hiyo ingewapa alama 3, na kuishia kutoa sare dhidi ya Osasuna.

 

Ancelotti Akataa Kumkosoa Benzema

Licha ya kurejea kwa Benzema baada ya kuumia kwa muda wa wiki tatu, Madrid walishindwa kupata alama tatu nyumbani kwao siku ya Jumapili ambapo bao lao la kuongoza lililofungwa na Vinicious Junior lilisawazishwa.

Benzema alipata nafasi ya kuifungia Madrid ushindi wa saba mfululizo wa ligi wakati David Garcia alipotolewa kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu mbaya lakini nyota huyo wa Ufaransa alikosa penati hiyo.

Ancelotti Akataa Kumkosoa Benzema

Ancelotti alikataa kumlaumu Benzema kwa matokeo hayo, hata hivyo, na kusisitiza Madrid haikufanya vibaya, akiiambia DAZN: “Karim huwa anafunga”. Kocha huyo anasema kuwa  mechi haikuwa ya kuvutia, lakini baada ya kusawazishiwa goli timu yake ilicheza kama ilivyotakiwa kucheza.

Ancelotti ameongezea kwa kusema kuwa Benzema hakuwa na matatizo ya kuanza kucheza dakika 90 na anatakiwa kuwa katika hali nzuri zaidi kwa kucheza. Matokeo hayo waliyopata jana amewafanya wapinzani wao wakubwa Barcelona kupanda hadi kileleni kwa kutofautiana magoli ya kufungwa na kufunga.

Ancelotti Akataa Kumkosoa Benzema

Real Madrid atamualika Shakhtar Donetsk siku ya Jumatano katika michuano ya Klabu Bingwa huku akiwa anaongoza kundi F akiwa na alama 6 baada ya kushinda mechi zake zote mbili za mwanzo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa