Safari ya Eden Hazard kuondoka Uingereza kama staa anayetegemewa zaidi hadi kuwa nyota abayetupiwa lawama zaidi Real Madrid, inaweza kuwa kuonekana kama hadithi, lakini ndiyo uhalisia.

Staa huyu amekumbwa na majeraha sana tangia kuwasili Real Madrid, kiasi cha kushindwa kutoa mchango uliofikia matarajio ya mashabiki wengi wa Real Madrid na wapenzi wengine wa soka.

Staa huyu aliyeonekana kupoteza radha na kushuka kiwango ukifananisha na alipokuwa EPL, amekuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo, huku vilabu kadhaa vikitajwa kuhitaji huduma yake.

Hata hivyo, bosi Carlo Ancelotti amebainisha kuwa staa huyu atasalia klabuni hapo.

“Mpango wake uko wazi kabisa. Anasalia na anafanya hivyo akiwa na motisha kwa kuwa amekuwa na wakati mgumu kwa miaka hii ya mwisho. Anataka kuonesha ubora wake.” – Carlo Ancelotti akimzungumzia Eden Hazard


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa