Sampdoria imeachana na kocha wake mkuu Marco Giampaolo baada ya kichapo cha mabao 3-0 Jumapili nyumbani dhidi ya Monza.

 

Sampdoria Yamtimua Kocha Wake Marco Giampaolo

Timu hiyo imefungwa na Monza timu ambayo ilikuwa ainaitia wakati mgumu kupata matokeo ambapo ushindi huo ni wapili kuupata toka wapande ligi kuu ya Italia, na mechi ya kwanza kushinda ni ile waliyomfunga Juventus.

Kocha huyo wa zamani wa Milan na Torino hatimaye alitimuliwa kibaruani yake baada ya mabao ya Matteo Pessina, Gianluca Caprari na Stefano Sensi kulaani Samp kwa kipigo kikali dhidi ya Monza aliyepanda daraja kwenye Uwanja wa Luigi Ferraris.

Huku taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo ilisema: “Sampdoria imetangaza kuwa imemwachia kazi kocha Marco Giampaolo”. Wakisema kuwa klabu ingependa kumshukuru Marco na wafanyakazi wake kwa kujitolea na weledi waliuonyesha wakati wakifanya kazi na Sampdoria.

Sampdoria Yamtimua Kocha Wake Marco Giampaolo

Timu hiyo inayoshikilia mkia kwenye msimamo wa Serie A itasafiri kwenda Bologna siku ya Jumamosi kukipiga kwenye mchezo wa raundi ya 9 dhidi ya Bologna.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa