Mkurugenzi uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, amefunguka kuwa shabaha yao katika usajili mkubwa walioufanya msimu huu ni kuhakikisha kikosi hicho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Akizungumza na Sports Arena [SA], Injinia Hersi [GSM] alisema:
” Tumekamilisha usajili wa Fiston, miongoni mwa washambuliaji bora zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
“Sisi kama GSM Shabaha yetu katika kufanya usajili huu ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi ambacho kitatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, na kupata nafasi ya Kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Wakati huohuo Kocha wa Yanga, Cedric Kaze, amezungumzia usajili wa Fiston akisema:
“Fiston ni chaguo na mapendekezo yangu, kwa hiyo kuja kwake kumekuja kunogesha falsafa yangu ambayo najaribu kuitengeneza.
“Yule anajua kufunga na anajua kutengeneza nafasi za mabao, namjua vizuri na amekuja kucheza kwenye kikosi cha kwanza, hivyo wapinzani wajiandae tu.”
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.
Magdalena
Wapambane Sana mpaka kufikia uko
Rahmal
Saw tunasubilia tuone
Adelta
Inapendeza 👏👏
Sabrina
Safi Sana tunatarajia owe hivyo
Sarah
Safi sana
warda
Watabebwa na simba tu hawa hawana mpango
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki wa yanga
Hopemwaikuka
Tutaonaa
felister
safi
Shakila mrope
Mhh yetu macho mashabiki
Mwanahamisi
Safi sana
Ernest Kimeru
Ngoja tuone, Tatizo mpira wa Bongo siasa nyingi ndani
Issa
Wape salam
Angelina
Utopolo tu
Lydia Emmanuel Magoti
Safii sana
Neema juma
Vizuri sana
Sania
Gsm hatutaki maneno tunataka vitendo