Kuelekea mashindano ya Chan 2021, Tanzania inaamini inauwezo wa kuwanyamazisha Zambia (Chipolopolo). Hii ni kwa mujibu wa Nadir Haroub “Cannavaro”.
Taifa Stars imepangwa kundi D kwenye mashindano ya Chan 2021 ambayo yatafanyika nchini Cameroon. Stars wataitupa karata ya kwanza siku ya Jumanne dhidi ya Zambia katika dimba la Limbe Omnisport.
Kuelekea mchezo huo, Stars wanaamini wanakila silaha ya kuwaangamiza Zambia ambayo inafundishwa na kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic. Imani hii ni baada ya Tanzania kudai wanazifahamu mbinu na namna ya uchezaji kwa timu yeyote iliyochini ya Micho.

Micho anahistoria ya kuvifundisha vilabu mbalimbali vya ukanda wa Afrika Mashariki na hii inawapa nguvu Stars kwa kuwa wanamfahamu vizuri katika ubora wake wa kuandaa timu.
Kwa mujibu wa Cannavaro ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Stars na sasa ni meneja wa kikosi hicho amesema, “ninamfahamu vizuri Micho. Alishawahi kunifundisha na ni kati ya makocha wanaotumia sana viungo. Timu yake inajengwa na viungo na anauzoefu wa kufundisha timu nyingi za Afrika Mashariki.
“lakini pia ninajua tunakocha mzuri, ameangalia video za namna Zambia inavyocheza na tutajipanga vizuri kupambana naye, tutajaribu kuzuia namna ya uchezaji wake, tunajua inawezekana.”
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.
Adelta
Wajipange wasije kujikuta wao ndiyo
Wanaenda kupigwa
warda
Sawa sie tunataka ushindi tu
Dorophina
Cha msingi ni kujipanga watawaangusha tu
Magdalena
Tanzania waongeze juhudi za kutosha ili wasonge mbali
Sabrina
Tanzania lazima amgalagaze mtu
Rahmal
Vizuli tanzania sisi tunataka ushindi
Hopemwaikuka
Kila la her kwao
felister
ushindi lazima
Mwanahamisi
Kila la kheri
Ernest Kimeru
Kazi kazi, Kila la kheri Tifa Stars
Issa
Kombe let tz
Angelina
Kila kheri Tz
Lydia Emmanuel Magoti
Kila la kheri timu yetu yataifa
Neema juma
TZ sio watu wamasiaraa aiseee
Sania
Kila LA kher Taifa stars
Caroline
Watajua hawajui