Baada ya Klabu ya Simba SC kumtangaza Thierry Hitimana (42), kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, amezungumzia nafasi aliyoipata na utayari wake katika kuitumikia klabu hiyo.

“Simba SC ni timu kubwa kwa sasa Afrika. Kupata nafasi ya kufanya kazi na klabu kama hii ni jambo la kujivunia na fursa kukuza experience yako.” alianza Hitimana.
“Unajifunza kufanya kazi na timu yenye uhitaji wa matokeo chanya katika kila mechi inayocheza kitu ambacho kama kocha kinakufanya muda wote kuwa stable kwenye mbinu zako.
“Kuwasoma wapinzani , kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji wako, saikolojia yako pia kuimarisha umoja wa timu na klabu mbele ya wanachama wetu, mashabiki na uongozi kwa ujumla.
“Tunajukumu kubwa kimataifa pamoja na boss wangu Gomes na hakika tutatimiza malengo ya timu na klabu “ aliongeza Hitimana.
Kwasasa Hitimana ameshajiunga na timu ya Simba SC iliyopo Jijini Arusha kwaajili ya kujiandaa na msimu ujao wa mashindano.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


