Joan Laporta Ashangaa Dembele Kubaki Barcelona

Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ashangaa Ousmane Dembele kuamua kubaki kwenye klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga kwenye klabu ya Barcelona kwenye dirisha lilifungwa jana alihusishwa na vilabu mbalimbali baada ya kutoelewana na klabu yake kwenye makubaliano ya mkataba mpya.

Joan Laporta
Joan Laporta

Katika harakati za kutotaka kumuachia aondekee huru majira ya kiangazi walitaka kuweza kupunguza mzigo wa mshara na wao japo wapate kitu ili asiweze kuondoka bure mwisho wa msimu japokuwa alihusishwa na vilabu vya Paris Saint Germain na Chelsea lakini mpango huo ulishindakana.

Joan Laporta ametoka na kumkosoa Dembele haileti maana ya yeye kubaki kwenye klabu hiyo, pia alinukuliwa akisema, “Tulimpa mapendekezo mawili na yalikuwa mazuri, lakini tunashangaa hakuyakubali.

“Moja lilikuwa kutoka kwenye klabu ya Uingereza lakini hakutaka kwenda alichagua kubaki hapa kwa miezi sita, si vyema yeye kubaki kwenye klabu, kwasababu kusaini kwake makataba mpya ungetupa ahueni ya bajeti ya mishahara.

“Timu ya Dembele ni ngumu kuielewa, Xavi anafanyia kazi kwa ajiri ya msimu ujao, tulifikilia kuwa Dembele ameshakubaliana na klabu nyingine, hivyo ndibyo wakala wake alivyotumbia.” alisema Joan Laporta.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe