Joseph Omog Kocha Mpya Mtibwa Sugar.

Klabu ya Mtibwa Sugar imemtangaza rasmi Joseph Omog kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kutoka Morogoro baada ya kocha Hitimana kuelekea Simba SC.

 

Siku ya jana ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru aliweka wazi kuwa tayari kocha Joseph Omog amepewa majukumu kuinoa Mtibwa Sugar.

Awali majukumu ya kuinoa Mtibwa Sugar ilibidi yawe mikononi mwa kocha Hitimana lakini alijiunga na mabingwa wa Tanzania, Simba SC kabla ya kusaini mkataba na timu hiyo.

Kifaru amesema kuwa ni maombi zaidi ya makocha 72 walikuwa nayo mkononi ila wao waliweza kufanya mchujo wao na kufika makocha watano na hatimaye sasa ni Omog atakuwa mbeba mikoba iliyoachwa wazi na Hitimana.

Joseph Omog ambaye ni raia wa Cameroon amewahi kuifundisha Azam FC, AC Leopards na Simba SC hivyo ana uzoefu mkubwa na soka la Tanzania.


FUNGA BAHATI YAKO NA MERIDIANBET.

Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe