Ripoti kutoka Italia zinadai kuwa Juventus wamefikia makubaliano ya kumsajili Nico Gonzalez kutoka Fiorentina kwa Euro milioni 30, lakini Tuscans hao wanapaswa kusajili mbadala wake kabla ya kumpeleka Muargentina huyo Turin.

La Gazzetta dello Sport na Il Corriere dello Sport zinadai kwamba klabu hizo mbili tayari zimepeana mikono, lakini Fiorentina wanataka kumsajili Albert Gudmundsson kutoka Genoa kabla ya kutoa mwanga wa kijani.
Juventus wamefikia makubaliano ya kumsajili Nico Gonzalez kutoka Fiorentina
Nico tayari amekubali masharti binafsi na Bibi Kizee na yuko tayari kusaini kandarasi ya €3.5m kwa mwaka.

Wakurugenzi wa klabu Cristiano Giuntoli (Juventus) na Daniele Pradé (Fiorentina) walikutana mjini Forte dei Marmi (Tuscany) siku ya jana ili kukamilisha mpango huo. Giuntoli hakufuata timu Sweden, ambapo vijana wa Thiago Motta walipoteza 2-0 dhidi ya Atletico Madrid.
Kwa mujibu wa magazeti yote mawili, Juve na Fiorentina pia wanajadili kuhusu mikataba zaidi.


