Klabu ya Juventus iliyo chini ya kocha Max Allegri imeripotiwa kupeleka ombi la mkopo kwa klabu ya Manchester City ikimtaka mshambuliaji Gabriel Jesus.
Benchi la ufundi la Juventus linaamini kuwa Jesus atapeleka kitu tofauti kwenye timu hiyo akiungana na wakali kama Ronaldo, Dybala na Alvaro Morata.
Manchester City wameweka dau la pauni milioni 60 mpaka 65, lakini Juve hawapo kwenye nafasi ya kutoa dau hilo licha ya kuwa na uhitaji.
Hivyo katika ombi hilo wamesalisha pia uwezo wa kumnunua moja kwa moja msimu ujao endapo atafika klabuni hapo kwa mafanikio.
Jesus sio chaguo la kwanza la Pep Guardiola huku akifunga magoli 14 tu katika michezo yote 43 ya City kwa msimu uliopita.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!



Issa
Safi