Kocha mpya wa Tottenham Nuno Espirito Santo amedai kuwa Harry Kane bado ni mali ya timu hiyo na hauzwi kama ilivyodaiwa na kuvunja matumaini ya Chelsea na City.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wake wa kwanza Nuno amedai kuwa Kane ni mchezaji bora sana na yeye anaamini bado ni mali ya Tottenham na hawezi kuuzwa kutokana na umuhimu wake klabuni hapo.
Katika mazungumzo hayo, Nuno pia alieleza ukweli kuwa mchezaji huyo ni tegemeo la timu hiyo kuelekea msimu wa 2021/2022 na kwa pamoja wana malengo makubwa wanayotaka kufikia.
Kane yupo katika mapumziko baada ya kutoka kwenye majukumu ya kimataifa akiwa na Uingereza na kocha huyo na anamtakia arejee katika utimamu wake wa mwili mapema na baada ya hapo watazungumza kuhusu kuongeza mkataba.
Miezi kadhaa nyuma mchezaji huyo alieleza kutamani kuondoka klabuni hapo na kwenda kutafuta changamoto kwenye klabu zitazoshiriki klabu bingwa ulaya msimu ujao zikiwemo Chelsea na Man City.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!
Issa
Kane mnyama