Arsenal Yamtaka Abraham Darajani.

 

Mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham anaonekana kuwa njiani kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto, na ripoti za hivi karibuni zinadai Arsenal wanavutiwa na usajili wake kulingana na Telegraph.

 

Abraham, 23, amekuwa akitafuta nafasi katika kikosi cha kwanza tangu Thomas Tuchel achukue madaraka kutoka kwa meneja wa zamani wa Blues na gwiji wa klabu hiyo Frank Lampard mwishoni mwa Januari.

Timu nyingi zimekuwa zikitaka kumsajili mchezaji huyo wa Chelsea ikiwemo Aston Villa, Leicester City na klabu ya West Ham wote wanahusishwa na mshambuliaji huyo wa kutaka.

Arsenal inahitaji kulipa pauni milioni 40 kuweza kupata saini ya mshambuliaji huyo kinda, pesa inayodhaniwa kuwa inaweza kuwakatisha tamaa washika mitutu hao wa London.

Ikumbukwe Abraham alikaririwa msimu uliopita kwamba familia yake yote ni mashabiki wa Arsenal na yeye pekee ndiye shabiki wa Chelsea baada ya kuifunga klabu hiyo.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

2 Komentara

    Aende

    Jibu

    Aende

    Jibu

Acha ujumbe