Timu ya Leeds United imethibitisha timu mbili kubwa itakazocheza nazo kuelekea maandalizi ya msimu ujao wa 2021/2022.
Leeds watacheza mchezo wao kwanza wa kirafiki dhidi ya Real Betis kutoka La Liga tarehe 31 mwezi katika uwanja wa chuo kikuu cha Loughborough nchini Ungereza na tiketi za mechi hiyo zishawekwa mtandaoni.
Baada ya hapo, Leeds United watalazimika kusafiri kwenda mpaka Amsterdam kwa ajili ya kucheza na mabingwa wa ligi ya Uholanzi FC Ajax mnamo tarehe 4 mwezi wa nane mwaka huu, lakini mechi hii haitakuwa na mashabiki kwa sababu ya Covid 19.
Mpaka sasa Leeds wamethibitisha kuwa na michezo mitano ya maandalizi ya msimu ujao, timu nyingine walizokubaliana nazo ni Guiseley AFC, Blackburn Rovers na Fleetwood Town ambazo zote zitachezwa mwezi julai.
Leeds United wanategemewa kuanza kutimua vumbi msimu wa 2021/2022 dhidi ya mashetani wekundu, Manchester United, tarehe 14 mwezi huu.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!



Ernest
Leeds chama kubwa, Msimu wa 2021/2022 lazima wapindue Meza
Issa
Leeds wapo poa