Imethibitishwa kwamba winga wa West Ham Felipe Anderson ameachana na klabu hiyo na kurejea Lazio.

Mchezaji huyo alijiunga na timu ya Premier League akitokea Lazio mwaka 2018 kwa dili iliyokuwa na thamani ya £34 million ($44m).
Lakini mchezaji huyo wa miaka 28 ametumia msimu uliyopita na klabu ya Porto kwa mkopo na imethibitika kurudi tena katika Serie wakati huu wa majira ya joto.
Anderson alitua Italia siku ya Jumanne kukamilisha dili hiyo ya kurejea na klabu ya Lazio iliweka picha ya mchezaji huyo akiwa amevaa skafu yao kwenye media ya kijamii.

Ujumbe kwenye tovuti ya West Ham ulithibitisha kwamba dili hiyo imekwishafanyika na Lazio kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao 12 katika michezo 72 kwa timu hiyo ya London.
Alikuwa akipangwa kwenye timu ya kwanza katika msimu wake wa kwanza na klabu akicheza mechi 40 kwenye mashindano yote.
Lakini alitumia msimu wa 2020-21 na Porto ya Ureno kwa muda muda mfupi na aliichezea timu hiyo michezo 10 tangu Oktoba iliyopita.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!



Ernest
Anderson hakuwa na msimu mzuri ndani ya Westham
Issa
Hana maajabu
Sarah
Hana jipya