Afisa Mkuu Mtendaji wa Liverpool, Peter Moore anatazamiwa kuondoka rasmi uwanjani Anfield mwishoni mwa Agosti 2020 baada ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Nafasi ya Moore itatwaliwa sasa na Billy Hogan ambaye kwa sasa ni mkurugenzi msimamizi na afisa mkuu wa masuala ya kibiashara kambini mwa Liverpool.

 

Liverpool Kuagana Rasmi na Mtendaji Peter Moore.

Kwa miaka mitatu iliyopita, More ameshuhudia Liverpool wakirejea katika ubora wao wa zamani kiasi cha kujinyanyulia ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya miaka 30 ya kusubiri, ufalme wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na Kombe la Dunia la FIFA.

“Haya ni mafanikio makubwa ambao tumeongozwa na kocha Jurgen Klopp, wachezaji na maafisa wetu wote katika benchi la kiufundi kupata.

Kikosi cha Liverpool kimerejesha hadhi yake ya zamani na kwa sasa ni tishio kubwa kwa mpizani yeyote barani Ulaya na duniani,” akasema Moore.

“Hizi ni kumbukumbu zitakazodumu kwangu milele. Kwa kweli tulistahiki kutamba jinsi tulivyofanya baada ya kufanya yote tuliyoyafanya!” akaongeza kinara huyo.

 

Liverpool Kuagana Rasmi na Mtendaji Peter Moore.

Hadi kutua kwake kambini Anfield, Moore ambaye atarejea kwao Amerika, aliwahi kuwa mfanyakazi wa masuala ya teknolojia katika kampuni za Sega, Microsoft, EA Sports na Reebok ambayo hutengeneza vifaa vya michezo.

“Nilikuja Liverpool mnamo 2017 baada ya kuhudumu Amerika kwa zaidi ya miaka 30. Nimekuwa na kipindi spesho sana uwanjani Anfield,” akasema Moore.


Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure.
Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.

Cheza Hapa Sasa

37 MAONI

  1. Sifa za Mtendaji Mkuu wa Timu ni kusikiliza ushauri wa bench la ufundi na kuifanyia kazi. Pale bench la ufundi linapotaka mchezaji fulani kazi ya mtendaji mkuu ni kuwezesha hilo kufanyika. Nadhani Peter Moore ameshirikiana nae na wenzie vizuri ndio maana timu imepata mafanikio hayo#meridianbettz

  2. Hizi ni kumbukumbu zitakazodumu kwangu milele. Kwa kweli tulistahiki kutamba jinsi tulivyofanya baada ya kufanya yote tuliyoyafanya!” akaongeza kinara huyo.

  3. Peter Moore amefanya vizuri ushirikiano na wezake katika timu hiyo na kuleta mafanikio ya kupata ubigwa nafikiri ni juhudi walizotumia kwa pamoja

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa