Kufuatia usajili wa moja kwa moja wa Philippe Coutinho kuendelea kubaki Bayern Munich kukwama. Sasa Barcelona wanatafuta suluhisho la mchezaji huyo ambaye anaonekana hana namba katika kikosi chao kwa sasa.
Vilabu mbalimbali vimekuwa vikihusishwa na usajili wa Coutinho kwa siku za hivi karibuni. Chelsea, Man United, Totenham na Arsenal ni kati ya vilabu vinavyotajwa kuisaka saini ya mbrazili huyo.

Taarifa zilizopo kwa sasa ni kwamba Arsenal na Totenham ndio timu zilizobaki katika kuwania saini ya Coutinho ambaye pia anaona nafasi ya kurudi tena kunako Ligi Kuu Uingereza – EPL baada ya kuiacha Liverpool miaka kadhaa iliyopita, ni fursa ya kipee kwake.

Inasemekana Arsenal wamejipanga kumtoa kiungo wao Matteo Guendouzi na kiasi cha fedha takribani pauni milioni 9 ili kumsajili Coutinho.Ofa hii inaonekana itasaidia pande zote mbili – Arsenal na Barcelona ambao wachezaji hawa wanaonekana kutokuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya vikosi hivi.
Uongozi wa Arsenal unasubiri kuiona hatma ya Arsenal katika fainali ya Kombe la FA watapokutana na Chelsea. Endapo Arsenal watafanikiwa kunyanyua kombe hilo, watakuwa katika nafasi nzuri kiuchumi na hivyo bajeti ya usajili itaongezeka kwa kiasi fulani.
Arteta bado anakuwa mwenye mashaka katika hili kwani Juventus nao wanaonekana kuitafuta saini ya Guendouzi. Japokuwa, Arsenal mpango wao wa kubadilishana wachezaji bado upo palepale.Kwao (Arsenal) hii ndio njia pekee ya kuendana na madhara ya kiuchumi yaliyosababishwa na Mlipuko wa Virusi vya Corona duniani.

Arteta anamtizama Coutinho kama mchezaji mwenye faida zaidi kulingana na mfumo wake wa kiuchezaji. Anamtizama Coutinho kama mrithi wa Pierre-Emerick Aubameyang endapo mshambuliaji huyo ataamua kuondoka Emirate.

Pia, hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya usajili wa Dani Ceballos anayechezea Arsenal kwa mkopo akitokea Real Madrid, inamuongezea mashaka Arteta katika nafasi hiyo. Endapo Ceballos ataamua kuondoka, Arteta atakosa mtu wa kuziba pengo hilo na hivyo Coutinho kuwa usajili wenye faida zaidi kwa Arsenal.
Arsenal watakuwa uwanjani leo kukipiga dhidi ya Chelsea katika fainali ya Kombe la FA. Ushindi kwa Arsenal ni faida kiuchumi, lakini pia itawapa tiketi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Europa msimu ujao.
Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure. Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.


Caroline
Arteta anamtazama Countino Kama mchezaji mwenye faida
Tatu
Chelsea, arsenal, Tottenham wanatakiwa kujipanga kwenye pesa ndio atamchukua countinho
Rehema
Bonge la makala
Ernest
Coutinho kama atatua Arsenal itakuwa deal zuri sana kwa Arsenal anaweza wasaidia kuleta ushindani zaidi.
Zeiyana
Hitakua vizuri kama arsenal wakimsajili acountinho
Lydia Emmanuel Magoti
Jembe Hilo acontinho Arsenal msilaze damu kwa jembe hilo
Shafii
Continho Hana bahati kabisa ila ni mchezaji mahili Sana.
felister
bora coutinho angekuja zake arsenal arteta amuangalie kwa jicho la tatu
Adelta
Asante kwa makala nzuri #
Meridianbettz
Isaya massawe
Coutinho amekua hana bahati kabisa
Magdalena
Coutinho nyota yake Kama imezimika tofauti na alivyokuwa akiwika mwanzo
Ester mmakasa
Kila lakheri kwa arsenal maana bado hawako vizuri .
Povel
Countinho Kama atafanikiwah kwenda Arsenal ni sawa Kama kazima ndoto zake kuchukuwah mataj na kuchukuwah uchezaj Bora wa dunia vle
Rose kapinga
Arsenal fanyen kwel msilaze damu!!!
Samiah
Makala yakijanjaa
Sadick
Maisha yanabadilika haraka sana Countinho kutoka kuwa nyota akiwa Liverpool hadi kutakiwa kuondoka ktk Klabu kwasababu ya kiwango duni#meridianbettz
Issa
Arsenal bado kwa courtinho
aisha
Coutinho yuko vizuri sana
Samira
Coutinho yupo vizuri
Dorophina
Itakuwa poa kama Coutinho ataenda arsenal hilo ni bonge la dili
Mwajumah
Asante kwa makala
Amani
Me naona Bora asalie kwenye timu yake ya Sasa kuliko kwenda utopoloni# meridianbettz
Khadija
Bonge la makala#meridianbettz
Fatina mfingi
Makal nzur
Furahav
Hatari s
Devotha
Dili likikamilika la coutinho kwenda arsenal itakua vizuri sana
Hope mwaikuka
Axante kwa taarifa nzur
Gabriel
Habar njema
Amiri Kayera
Nic
Tahiya
Good news
Saupha mohamed
Good news
Latifa juma mohamed
Nmefurahishwa na makala poa Sana.
Theonestina
Asanteni meridianbet kwa makala nzuri
Leonard
Itakuwa vizuri akija arsenal
Flomena
Yuko vizuri kijana Arsenal wafanye kuweka dau kubwa mezani
Ester jackson
courtinho ni mchezaji mzuri la kuelekea arsenal mm naona ni Bure sana mana kuhama Liverpool ni sawa saw a na kiwango chako kimeshuka
Genia Sikaluzwe
Ahsant sana meridianbet kwa taarifa
Sabrina
Arsenal msilaze damuuu
farida ahmadi
Arsenal wamchukue countino ni mchezaji mzuri Sana pia hataongeza nguvu katika kikosi pia countino hatarudi tena kukicheza katika ligi ya premier
Theckla
Habari njema
David Pere
History ilikuwa inaonyesha kabisa kuwa watamchukua kombe la FA
Mwanahamisi
Gud news
Asia Abdy
I wish coutinho aende Arsenal atafanya meng mazur
warda
Habari nzuri sana