Liverpool Yapata Pigo Jingine

Klabu ya Liverpool imepata jingine ndani ya klabu yao baada ya kupata majeraha kwa beki wake muhimu ndani ya klabu hiyo Ibrahim Konate ambaye imeripotiwa atakaa nje ya uwanja wiki mbili mpaka tatu.

Klabu ya Liverpool ndani ya msimu huu imekua na wakati mgumu sana katika mashindano yote ambayo wamekua wakishiriki msimu huu na sababu kubwa ambayo inaelezwa kusababisha klabu hiyo kupitia kipindi kigumu ni majeraha ambayo wachezaji wake wamekua wakiyapata.liverpoolKlabu hiyo imekua na wimbi kubwa la majeraha na wachezaji wake muhimu mpaka sasa wako kwenye kitandani kutokana na majeraha. Wachezaji kama Luis Diaz, Diogo Jota, Virgil Van Dijk, na sasa Ibrahim Konate ambao ni wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo.

Ibrahim Konate amekua msaada mkubwa sana ndani ya klabu ya Liverpool ndani ya siku za karibuni hivo kupata majeruhi kwa mchezaji huyo kunaacha pengo kubwa ndani ya klabu ya hiyo, Kwani beki mwingine mwenye ubora ndani ya timu hiyo Virgil Van Dijk akiwa majeruhi.liverpoolImekua anguko la ghafla kwa klabu ya Liverpool msimu huu baada ya kuonekana hawana nafasi ya kubeba taji lolote ndani ya msimu huu, Huku msimu uliomalizka wakiwa kwenye ubora mkubw ana kushindania kila taji na wakiwa nafasi ya kubeba taji msimu uliomalizika na sababu kubwa ikitajwa ni majeraha ambayo yamekua yakiwaandama ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.